Home Habari za michezo RASMI….SIMBA WAACHANA NA MANZOKI….WAAMUA KUKOMAA NA ‘MZUNGUU’..WADAI DILI HALIKO WAZI PANDE ZOTE…

RASMI….SIMBA WAACHANA NA MANZOKI….WAAMUA KUKOMAA NA ‘MZUNGUU’..WADAI DILI HALIKO WAZI PANDE ZOTE…


Meneja wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema klabu hiyo imeamua kuachana na dili la kumsajili mshambuliaji nyota wa Vipers United ya Uganfda, Cesar Manzoki kutokana na sintoifahamu katika mkataba wake.

Kauli hiyo ya Ahmed inakuwa ikiwa ni baada ya maneno mengi ya mashabiki wanaodai kuwa Simba kwa sasa hawana mshambuliaji mzuri hata Dejan raia wa Serbia aliyesajiliwa hivi karibuni, hana uwezo ule uliotarajiwa.

“Cesar Manzoki jambo lake halipo wazi yeye mwenyewe anasema anamkataba ambao umesalia miezi miwili, huku klabu yake ikisema bado anamkataba wa miaka miwili, sisi kama Simba tumeamua kuachana na dili hilo na kufunga usajili wa Dejan ambaye tunaamini atatusaidia.

“Sababu iliyofanya tupoteza mchezo ni ubora wa Yanga waliokuja nao kipindi cha pili, sisi tulifanya vizuri kipindi cha kwanza na tukaweza kupata bao na wao wakaja kipindi cha pili walibadilisha mbinu na wachezaji, tofauti na sisi tuliobadilisha watu lakini sio mbinu,” amesema Ahmed Ally.

SOMA NA HII  SABABU ZA SIMBA KUSHINDWA KUIFUNGA KAIZER CHIEFS DAR