Home Habari za michezo ABDI BANDA AKINUKISHA LIGI KUU AFRIKA KUSINI…AWAONYESHA KAZI CHAFU ORLANDO PIRATES…

ABDI BANDA AKINUKISHA LIGI KUU AFRIKA KUSINI…AWAONYESHA KAZI CHAFU ORLANDO PIRATES…


Beki wa Kimataifa wa Tanzania Abdi Banda anaeichezea klabu ya Chippa United ya nchini Afrika ya Kusini amefunga bao lililoipa ushindi klabu yake dhidi ya Klabu Kubwa ya Orlando Pirates.

Mechi hiyo ya Ligi Kuu ya Afrika ya Kusini iliamuliwa na goli la lala salama la Banda alilofunga dakika ya 85 na kuihakikishia Chippa United kuondoka na alama tatu.

Banda amewahi kuvichezea vilabu mbali,bali ndani na nje ya nchi kama vile Simba SC, Mtibwa lakini pia amewahi kucheza Afrika ya Kusini klabu ya Baroka FC.

SOMA NA HII  ZORAN : TIMU YENYE MALENGO MAKUBWA HUWAPA MAKOCHA MKATABA MREFU...SIMBA WAMENIPA MWAKA MMOJA TU...