Home Habari za michezo ZORAN : TIMU YENYE MALENGO MAKUBWA HUWAPA MAKOCHA MKATABA MREFU…SIMBA WAMENIPA MWAKA...

ZORAN : TIMU YENYE MALENGO MAKUBWA HUWAPA MAKOCHA MKATABA MREFU…SIMBA WAMENIPA MWAKA MMOJA TU…


KOCHA mpya wa Simba, Zoran Manojlovic amesema mkataba wa mwaka mmoja aliopewa na uongozi wa timu hiyo sio kitu kibaya kwake kwani sehemu zingine wanatoa mkataba wa miezi sita.

Zoran amesema hayo wakati akitambulishwa mbele ya Waandishi wa Habari katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa babari, Zoran amesema kwa uzoefu wake wa kuishi Ulaya, timu yenye malengo makubwa inawapa makocha wake mikataba ya miaka angalau minne jambo ambalo ni tofauti na Afrika.

“Nina uzoefu wa soka la Afrika huwa wanatoa mkataba wa miezi sita, huu wa mwaka mmoja ni mzuri japokuwa itanichukua hata miezi sita kwanza kujua namna ambavyo soka la hapa linavyokwenda,” amesema Zoran.

Zoran amesema anaifahamu Simba baada ya kuiona kwenye Mashindano ya CAF na hata aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Didier Gomes alikuwa anamfatilia vizuri.

“Naijua Simba kwa sababu nimeona mechi zao za CAF, Yanga naijua kidogo sana maana sijawahi kuona mechi zao,” amesema Zoran na kuongeza;

“Kocha wa zamani Simba, Didier (Gomes) nilikuwa nae Ligi ya Sudan na nilimfungua ila ni kocha mzuri sana,” amesema Zoran.

Zoran amepita katika timu mbalimbali Afrika kama Wydad Ac (Morocco), Al Hilal (Sudan), na CR Belouizdad 

SOMA NA HII  TRY AGAIN : MSIMU UJAO SIMBA SC TUTAKUWA NA KIKOSI BORA ZAIDI