Home Habari za michezo BALAAH LA MUDATHIRI YAHAYA LAWAFUNIKA VIUNGO WOTE LIGI KUU…TAKWIMU HIZI HAPA…

BALAAH LA MUDATHIRI YAHAYA LAWAFUNIKA VIUNGO WOTE LIGI KUU…TAKWIMU HIZI HAPA…

Habari za Yanga

Kiungo mpya wa Yanga, Mudathir Yahaya Abbas ameweka rekodi katika Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kucheza pasi nyingi zaidi wakati wa mchezo wao dhidi ya Ruvu Shooting.

Katika mchezo huo uliopigwa juzi Jumatatu, Januari 23, 2023, Wananchi waliibuka na ushindi wa bao 1-0 na kuendelea kujikita kileleni mwa ligi hiyo wakiwa na alama 56 mbele ya watani wao wa jadi, Simba wenye pointi 50.

“Kwenye mchezo wa Yanga dhidi ya Ruvu Shooting, kiungo wa Yanga Mudathir Yahaya alipiga jumla ya pasi 118,pasi 107 zilienda kwa usahihi huku pasi 11 hazikufika kwa walengwa.

“Pasi 118 ni pasi nyingi sana na hakuna mchezaji aliewahi kupiga pasi nyingi hivi kwa wachezaji wa Simba,Yanga na Azam Fc kwa msimu huu,” hii ni kwa mujibu wa Mzee wa Takwimu, Anuary Binde ambaye ni Mtangajazi wa Wasafi TV.

SOMA NA HII  ISHU YA BACCA NA YANGA YAZIDI KUVUMA....APEWA MBINU ZA KUNG'ANG'ANIA JAMBO LAKE...