Home Yanga SC MITAMBO YA MABAO YAANZA KAZI RASMI YANGA

MITAMBO YA MABAO YAANZA KAZI RASMI YANGA


 MITAMBO ya mabao ndani ya kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze tayari imeanza kazi kujiweka sawa kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na mashindano mengine.

Yanga ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa inashikilia rekodi ya kukamilisha mzunguko wa kwanza bila kupoteza mchezo.

Imecheza jumla ya mechi 18, imeshinda 13 na kulazimisha sare mechi 5 zinazowafaya wawe na pointi 44 kibindoni.

Mtambo wao wa mabao ambao ulifunga bao la kwanza ndani ya Yanga kwa msimu wa 2020/21 ni Michael Sarpong raia wa Ghana yeye jumla amefunga mabao manne kati ya 29 ambayo yamefungwa.

Nyota huyo alikwenda Ghana kwa ajili ya mapumziko mafupi ila kwa sasa tayari amesharejea ndani ya kikosi hicho ambacho kilianza mazoezi Januari 25, Kigamboni.

Ameungana na mshambuliaji mpya Fiston Abdulazack ambaye amepewa jina la kuwa ni mtambo wa mabao ndani ya Yanga.

meneja wa Yanga Hafidh Saleh amesema kuwa maandalizi yapo sawa na kila mmoja anafanya kile ambacho anaambiwa na mwalimu.

“Wachezaji wetu tayari wameanza mazoezi ikiwa ni kwa ajili ya kujiweka sawa na ligi tupo tayari na tunaamini kwamba tutafanya vizuri,” amesema.

SOMA NA HII  YANGA YAMPIGIA HESABU NDEFU MTAMBO WA MABAO MZAWA