Home Yanga SC KAZE AOMBA KIKAO NA VIONGOZI YANGA KISA SAIDO, JOB

KAZE AOMBA KIKAO NA VIONGOZI YANGA KISA SAIDO, JOB


KOCHA mkuu wa klabu ya Yanga, Cedric Kaze ameonyeshwa kukerwa na uamuzi wa nyota wake wawili, Dickson Job na Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ kuitwa kwenye vikosi vya timu ya Taifa huku wakiwa bado wana majeraha na kuahidi kufanya kikao na viongozi wa Yanga ili kudhibiti hali hiyo.

Nyota hao hawajaichezea Yanga mchezo wowote tangu Januari mwaka huu, kutokana na majeraha ya misuli yaliyokuwa yakiwakabili.

Saido alijitonesha majeraha yake kwenye fainali ya kombe la Mapinduzi, huku Job yeye akiwa ameumia kwenye kambi ya Stars iliyokuwa ikijiandaa na michuano ya CHAN.

Akiwazungumzia nyota hao, Kaze amesema: “Ni jambo la kushangaza sana kuona kile ambacho kimetokea kwa wachezaji wangu, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ na Dickson Job.

“Mpira ni mchezo wa wazi na kila mtu aliona ya kwamba Saido hakucheza tangu Januari 13, baada ya kupata majeraha kwenye kombe la Mapinduzi, hivyo ni takribani miezi miwili imepita hajacheza.

“Walipaswa kutuuliza kuhusu maendeleo yake kabla ya kumuita lakini hawakufanya hivyo, hii pia ni kesi moja na Job ambaye alipata majeraha akiwa na kikosi cha Stars mwezi Januari mwaka huu, wakati wakijiandaa na CHAN.

“Ikatubidi sisi tumhudumie mpaka alipopona, akiwa ndiyo kwanza amefanya mazoezi mara mbili pekee, unashangaa naye anaitwa timu ya Taifa bila kutupa taarifa.

“Kuhusiana na hili ni lazima nizungumze na viongozi wangu ili kurekebisha hali hiyo, sisi tunatumia nguvu kubwa kuwalinda wachezaji wetu, lakini haiwi hivyo wanapokuwa hawapo nasi, hatuwezi kuendesha timu kama tupo miaka 20 iliyopita,”

SOMA NA HII  YANGA SC WAIFANYIA UMAFIA SIMBA KWA MUDATHIRI...WAMPA MKATABA WA FEI TOTO...