Home Yanga SC ULA UTATA KUHUSU UHALALI WA AUCHO NA YANGA…UMEFIKIA HATUA HII..MWENYEWE AVUNJA UKIMYA

ULA UTATA KUHUSU UHALALI WA AUCHO NA YANGA…UMEFIKIA HATUA HII..MWENYEWE AVUNJA UKIMYA


MZIKI umekamilika. Ndio, Yanga mziki umeenea na kilichobaki kwa sasa kazi imebaki kwa makocha tu baada ya staa wao wa mwisho katika kikosi chao kuingia kambini jana usiku mkubwa, kisha asubuhi tu akaliamsha fasta.

Kiungo mkabaji kutoka Uganda aliyekuwa ndiye pekee hajatimba kambini mjini Marrakech na kuzua maneno kwa baadhi ya mashabiki, Khalid Aucho amewasili ndani ya kambi ya Yanga juzi usiku tayari kuanza kazi akitokea kwao alikoenda mara tu baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili.

Aucho baada ya kuwasili juzi hakukuwa na muda tena kwani jana asubuhi alianza kazi rasmi kwa kukimbizwa mtaani kama wenzake katika programu maalum ya kujaza stamina.

Haikuishia hapo, kiungo huyo baadaye aliungana na wenzake katika ratiba ya mazoezi ya gym ikiwa ni ratiba ambayo wenzake wameifanya kwa mara mbili mfululizo.

Baada ya mazoezi hayo kocha wake, Nasreddine Nabi alikaa naye katika kikao kilichotumia dakika 7 wakiongea mambo mbalimbali wakiwa wawili tu na hakuna aliyesikia kipi walikuwa wakizungumza.

Mara baada ya kikao hicho wawili hao walionekana wakicheka kisha kugonga tano, kisha kuelekea katika chumba cha kupata kifungua kinywa sambamba na timu nzima katika hoteli yao ya Kenzi Farrah Rose Garden.

Kiungo huyo alisema kwamba kwa sasa yuko tayari kuanza kazi ndani ya timu hiyo huku akifurahia mapokezi mazuri kutoka kwa wachezaji wenzake na viongozi wa klabu na wale wa benchi la ufundi.

“Nipo na furaha kubwa kuwa hapa, niko tayari sasa kuanza maisha mapya ndani ya klabu yangu ya Yanga, wenzangu wamenipokea vizuri tuko kama familia, lakini pia hata makocha na viongozi wa klabu wamenipa ushirikaino na sasa kazi ni moja tu kuifanyia kazi Yanga,” alisema Aucho ambaye mapema kabla ya mbio za asubuhi wenzake walimkaribisha kwa staili ya kucheza muziki huku wakimzunguka kama ambavyo walifanyiwa wachezaji wengine.

SOMA NA HII  HII HAPA RATIBA KAMILI NA TEREHE KWA MECHI ZA YANGA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA...