Home Yanga SC HAJI MANARA:NINAPENDA VIKOMBE, NITAFANYA KAZI YANGA KWA NGUVU ZAIDI

HAJI MANARA:NINAPENDA VIKOMBE, NITAFANYA KAZI YANGA KWA NGUVU ZAIDI


 ALIYEKUWA Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara ametambulishwa rasmi kujiunga na Klabu ya Yanga baada ya kuachana na mabosi wake wa zamani ambao kwa sasa wanaye Kaimu Ofisa Habari, Ezekiel Kamwaga.

Manara ametambulishwa leo Jumanne, Agosti 24, 2021 na uongozi wa klabu hiyo wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa mikutano wa Serena Hotel jijini Dar es Salaam.

“Namshukuru Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema kwa kutujalia kukutana hapa siku ya leo katika jambo hili ambalo ni kubwa na linaloweza kutuonyesha standards ambazo tunapaswa kwenda nazo katika ufanyaji kazi.

“Mimi msemaji, nimejiunga na timu kubwa kuliko zote Afrika Mashariki na kati, tunakwenda kuchukua ubingwa, lazima tutengeneza confiedence. Nitafanya kazi zaidi ya punda mwenye njaa na kwa nguvu zaidi.

“Nimefanya kazi Simba kwa miaka takribani saba sasa kwa kadri nilivyojaliwa, huenda nilifanya vizuri kama na huenda kuna watu wamewachukizwa kwa hiki, lakini katika press yangu nilisema kama binadamu siwezi kuvumilia niliyofanyiwa.

“Wengine watasema leo Simba kesho Yanga, mimi ni professional, kama kocha au mchezaji, anaweza kwenda timu yoyote, mimi ni msemaji, nitangaze rasmi kwamba nimejiunga na klabu kubwa kuliko zote Afrika Mashariki na Kati. Huu ukubwa mnaousema ninao ni lazima nifanye kazi na klabu kubwa, klabu ambayo itanipa nafasi kushirikiana nao.

“Baada press yangu nilipotoka Simba zilikuja ofa nyingi, waliponiambia viongozi wa Yanga kwanza nilishangaa, wakaniambia sisi tunataka tufanye kazi na wewe, lakini baadae nikaona wako siriazi, sikujiuliza mara mbili.

“Mimi napenda vikombe, Yanga wakanieleza namna walivyosajili nafurahi kujiunga na klabu ambayo ninaamini itashinda kila taji msimu ujao,” .

SOMA NA HII  NYOTA WA YANGA KUKUNJA MAMILIONI ILI KUTWAA TAJI LA LIGI KUU BARA