Home kimataifa DUH1 LUNINI ATUMIA MIAKA MITATU KUHCEZA MECHI MBILI

DUH1 LUNINI ATUMIA MIAKA MITATU KUHCEZA MECHI MBILI


 IMEBAINIKA kwamba kipa wa Real Madrid, Andriy Lunini amecheza mechi mbili katika miaka mitatu ambayo ameitumikia ndani ya timu hiyo inayoshiriki La Liga.

Katika mechi hizo mbili ni masaa mawili pekee ameyatumia kucheza jambo ambalo linamaanisha kwamba nafasi yake ndani ya kikosi hicho ni finyu.

Alijiunga na Madrid mwaka 2018 hivyo mpaka sasa ikiwa ni 2021 ameyeyusha miaka mitatu ndani ya timu hiyo.

Katika mechi hizo ambazo ni mbili alikwama kufanya vizuri ambapo moja alishuhudia kikosi hicho kikiondoshwa kwenye michuano ya Copa del Rey.

Mkataba wa kipa huyo unatarajiwa kumeguka mwaka 2024.

SOMA NA HII  BEKI SILVA AANDALIWA MKATABA