Home Yanga SC SAIDO NTIBANZOKIZA AREJEA YANGA,TAYARI KUWAVAA KMC KWA MKAPA

SAIDO NTIBANZOKIZA AREJEA YANGA,TAYARI KUWAVAA KMC KWA MKAPA

 


JUMA Mwambusi, Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa kurejea kwa Saido Ntibanzokiza kumeongeza ari ya kupambana kwa wachezaji wenzake. 


Kiungo huyo mshambuliaji raia wa Burundi alikuwa nje ya uwanja akitibu majeraha ya mgongo na alipopona alijiunga na timu ya taifa ya Burundi kuwania kusaka tiketi ya kufuzu Afcon.


Tayari ndoto ya Burundi kufuzu Afcon imeyeyuka kama majirani zao Tanzania hivyo amerejea kuendelea na kazi ndani ya kikosi cha Yanga.

SOMA NA HII  MUDATHIRI:- TUMECHOKA KUONEWA NA SIMBA...