Home epl ARSENAL YASHAURIWA KUMUWEKA KANDO AUBAMEYANG

ARSENAL YASHAURIWA KUMUWEKA KANDO AUBAMEYANG

 


MIKEL Arteta,  Kocha Mkuu wa Klabu ya Arsenal ameshauriwa kumuweka benchi kwa muda mshambuliaji wake Pierre Emerick Aubameyang na kumuanzisha kikosi cha kwanza Gabriel Martinelli.

Ushauri huo umetolewa na mchambuzi wa masuala ya michezo, Martin Keown kupitia Daily Mail kutokana na mwendo wa nahodha huyo kuwa wa kusuasua kikosini humo.

Arteta ameongoza jumla ya mechi 50 akiwa Arsenal ila kiwango cha wachezaji wake imekuwa ni maji kupwa maji kujaa na alishuhudia kikosi chake kikipoteza kwa kufungwa mabao 3-0 dhidi ya Liverpool,  Uwanja wa Emirates. 

Keown amesema kuwa ni lazima Arteta afanye maamuzi magumu ya kumuweka kando kwanza Aubameyang na kumuanzisha kijana Gabriel kwa kuwa amekuwa na uwezo mkubwa ikiwa ataendelea kumtumia Auba atahatarisha ushindi wake.

Arteta baada ya kupoteza mbele ya Liverpool aliomba msamaha kwa mashabiki wa timu hiyo kwa kuwa alikuwa anaamini kwamba walikuwa na nafasi ya kupata pointi tatu muhimu.

SOMA NA HII  KADI NYEKUNDU HAIJAMFURAHISHA TUCHEL