Home Yanga SC NYOTA WAWILI YANGA WANAUMWA, WAVURUGA MIPANGO YA MWAMBUSI

NYOTA WAWILI YANGA WANAUMWA, WAVURUGA MIPANGO YA MWAMBUSI

 


NYOTA wawili wa kikosi cha Yanga kilicho chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mwambusi wamevuruga mipango ya kocha huyo kutokana na hali zao kutokuwa sawa kwa ajili ya mazoezi.

Yanga inaendelea na mazoezi katika kambi yao iliyopo Kigamboni kwenye kijiji cha Avic ikiwa ni kwa ajili ya maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho

Mchezo wake wa kwanza baada ya ligi kurejea kwa kuwa ilisimama kutokana na maombolezo ya aiyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli, inatarajiwa kumenyana na KMC Uwanja wa Mkapa ambapo ni mchezo wa ligi wakiwa na kumbukumbu ya kupata ushindi wa mabao 2-1 kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa nyota wawili ambao walikuwa kwenye mpango wa kocha ni pamoja na Michael Sarpong pamoja na Balama Mapinduzi ila hawajawa fiti.

“Kikosi kipo sawa isipokuwa Balama Mapinduzi na Michael Sarpong hawa kwa pamoja wanaumwa.

“Kocha alitaka kutumia maandalizi haya kuwanoa vilivyo ili Sarpong aje kuwa lulu katika safu hiyo lakini kilichotokea imemfanya kujisikia vibaya,” .

Yanga ipo nafasi ya kwanza kwenye ligi ikiwa na pointi 50 baada ya kucheza jumla ya mechi 23.

Chanzo:Spoti Xtra

SOMA NA HII  KUHUSU YA YANGA NA MAMBO YAKE....MSUVA AVUNJA UKIMYA..AMNYOOSHEA KIDOLE MAYELE...