Home Simba SC AKILI ZA GOMES WA SIMBA ZIPO KWA WATANI ZAKE WA JADI YANGA

AKILI ZA GOMES WA SIMBA ZIPO KWA WATANI ZAKE WA JADI YANGA


LICHA ya kwamba amekiongoza kikosi chake kutinga hatua ya robo fainali baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya AS Vita, Didier Gomes hesabu zake zipo ndani ya Ligi Kuu Bara kuhakikisha anaishusha Yanga kileleni.

 

Gomes ambaye msimu huu ana kibarua cha kutetea taji la Ligi Kuu Bara, Mei 8, mwaka huu atakutana na Yanga kwa mara ya kwanza tangu awe kocha wa Simba.

 

Kabla ya timu hizo kukutana, Simba itacheza mechi tano za ligi ambazo ni sawa na dakika 450, huku Yanga iliyo chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mwambusi, ikiwa na dakika 360, sawa na mechi nne


Mechi za Gomes ni dhidi ya Mtibwa Sugar (Aprili 14), Mwadui FC (Aprili 18), Kagera Sugar (Aprili 21), Gwambina (Aprili 24) na Dodoma Jiji (Aprili 27), kisha ndiyo anakutana na Yanga.

 

Kwa upande wa Mwambusi, yeye atakuwa na kazi mbele ya KMC (Aprili 10), Biashara United (Aprili 17), Gwambina (Aprili 20), Azam (Aprili 25), kisha atapambana na Simba ya Gomes.

 

Gomes raia wa Ufaransa, ameliambia Spoti Xtra kuwa: â€śMechi zote kwetu ni muhimu kupata pointi tatu, kwani ukitazama tunahitaji kuongoza ligi ili kufikia lengo la kutwaa kombe, haitakuwa kazi rahisi, nimewaambia wachezaji wana kazi kubwa ya kufanya,” .

 

Msimamo wa Ligi Kuu Bara kwa sasa unaonesha Yanga inaongoza ikiwa na pointi 50 baada ya kucheza mechi 23, huku Simba ikiwa ya pili ikikusanya pointi 46 ikishuka dimbani mara 20.

SOMA NA HII  KISA USHINDI WA JANA DHIDI YA RUVU...PABLO AANZA 'KUCHONGA'...AGUSIA IDADI YA MAGOLI...