Home Habari za Simba KIUNGO MNIGERIA AWAGOMEA SIMBA…MABOSI WACHANGANYIKIWA

KIUNGO MNIGERIA AWAGOMEA SIMBA…MABOSI WACHANGANYIKIWA

KIUNGO MNIGERIA AWAGOMEA SIMBA...MABOSI WACHANGANYIKIWA

Wakati Kiungo wa Simba raia wa Nigeria, Victor Akpan akiendelea kusaka namba katika kikosi cha Ihefu, ameiomba klabu yake impeleke Coastal Union.

Akpan alisajiliwa na Simba mwanzoni mwa msimu huu akitokea Coastal Union, lakini tangu atue hapo ameshindwa kuonesha uwezo wake jambo lililowafanya mabosi wa Simba kumpeleka Ihefu kwa mkopo kipindi cha usajili wa dirisha dogo.

Chanzo chetu kutoka Simba, kimesema kuwa, Akpan amegoma kusalia lhefu na badala yake ameuomba uongozi wa Simba umruhusu aende Costal ambako anaamini atapata nafasi kubwa ya kucheza.

“Mambo yanazidi kuwa magumu kwa Akpan kiasi kwamba amegoma kabisa kusalia Ihefu mwishoni mwa msimu huu, ameutaka uongozi wetu umruhusu arejee Coastal Union ili akapate namba ya kucheza kikosi cha kwanza,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kuzungumza na Kocha wa Ihefu, Zubery Katwila alisema: “Kwa sasa bado kuna wachezaji wengi tunaendelea kuwatazama uwezo wao kama sehemu ya maboresho ya timu yetu, hivyo mchezaji yeyote atakaonekana kufanya vema hatutakubali kumuachia.”

SOMA NA HII  TUZO YA SAKHO YAMPA MZUKA MO DEWJI....AIBUKA NA KUNENA HUYA KUHUSU SIMBA ....AGUSIA WACHEZAJI ...