Home Habari za Yanga YANGA YAMFUTA KAZI KOCHA WAO MKUU…KOCHA WA MUDA AKABIDHIWA TIMU

YANGA YAMFUTA KAZI KOCHA WAO MKUU…KOCHA WA MUDA AKABIDHIWA TIMU

YANGAKULITETEA TAJI LAO...TUMEWAACHA POINTI NYINGI WANAOTUFATA...TUNAPAMBANIA MATAJI YOTE

BAADA ya Yanga Princess kuonekana kusuasua kwenye Ligi ya Wanawake (WPL) msimu huu hatimaye viongozi wamefikia makubaliano ya pande zote mbili kuvunja mkataba na Kocha huyo.

Taarifa iliyotolewa leo na Ofisi ya Mtendaji Mkuu wa Yanga imeeleza kuwa kikosi hicho kwasasa kipo chini ya Kocha Fredy Mbuna mpaka pale msimu utakapomalizika huku sababu za kuvunja mkataba huo zikiwa hazijawekwa wazi.

“Uongozi wa Klabu ya Yanga unapenda kuutaarifu umma kuwa umefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa Timu ya Wanawake, Yanga Princess, Sebastian Nkoma”.

Nkoma alitambulishwa rasmi Desemba 10,2022 akitokea Simba Queens na uongozi wa klabu hiyo kufanya uamuzi wa kumtimua Kocha Mkuu Edna Lema na msaidizi wake Mohamed Hussein ‘Mmachinga’ baada ya timu hiyo kufungwa bao 1-0 na Fountain Gate Princess.

Kocha huyo aliifundisha Simba Queens kwa mafanikio makubwa na kuiwezesha kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Bara mara mbili mfululizo.

Hata hivyo kocha huyo aliondolewa Simba Queens baada tu ya kuipa ubingwa wa Cecafa kwa kuifunga She Corparate ya Uganda bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika Agosti 27.

SOMA NA HII  YANGA VS AZAM SIO POA KWA HALI HII LOLOTE LINAWEZA KUTOKEA