Home Uncategorized SIMBA IPO KAMILI GADO KUVAANA NA MBEYA CITY KESHO

SIMBA IPO KAMILI GADO KUVAANA NA MBEYA CITY KESHO


UONGOZI wa Simba umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho utakaochezwa Uwanja wa Sokone majira ya saa 10:00 jioni.

Akizungumza na Saleh Jembe, Meneja Mkuu wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa kila kitu kinakwenda sawa na wachezaji wapo tayari kwa ushindani.

“Wachezaji wanajua majukumu yao hakuna ambaye anafikiria kushindwa hivyo kazi kubwa kesho ni kusaka pointi tatu ndani ya uwanja, mashabiki wajitokeze kuona burudani,” amesema.

Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 75 baada ya kucheza mechi 30.

SOMA NA HII  KUHUSU MSIMU UJAO....BEKI YANGA AITAJA SIMBA..!!!