Home Uncategorized EXCLUSIVE: USAJILI WA BIGIRIMANA WAZUA MSALA YANGA, APR KUCHUKA HATUA ZA KISHERIA

EXCLUSIVE: USAJILI WA BIGIRIMANA WAZUA MSALA YANGA, APR KUCHUKA HATUA ZA KISHERIA


Katibu Mkuu wa APR ya Rwanda Adolphe Kalisa, amefunguka kwa kusema kuwa ameshangazwa na Yanga kwa kumsajili mchezaji wake Issa Birigimana bila kufuata taratibu.

Kalisa ameeleza kuwa ameshangazwa na klabu kubwa kama Yanga kufanya maamuzi hayo ili hali mchezaji huyo akiwa bado hajamaliza mkataba wake na APR.

Yanga umemtangaza Birigimana kuwa mchezaji wake kwa kusaini mkataba wa miak miwili utakaomalizika mwaka 2021.

“Tumeishangaa klabu kubwa Kama Yanga kumsajili mchezaji wetu Issa Birigimana ambaye bado ana mkataba mpaka 2020.

“Hatuna uhakika kama klabu hii ina katibu mkuu, hatua za kisheria zitafuata.”

SOMA NA HII  TSHISHIMBI AFUNGUKA HATMA YAKE NDANI YA YANGA