Home Habari za michezo FAILI LA MASTAA WAPYA NA WATAKAO TEMWA SIMBA HILI HAPA….MBRAZILI ‘KAKAZA SHINGO’...

FAILI LA MASTAA WAPYA NA WATAKAO TEMWA SIMBA HILI HAPA….MBRAZILI ‘KAKAZA SHINGO’ AISEE..

Habari za Simba SC

Taarifa za ndani kutoka Klabu ya Simba zinaeleza kuwa, ripoti ya Kocha Mkuu, Roberto Oliveira kwa bodi ya wakurungezi wa klabu hiyo inataka usajili wa wachezaji nane wapya ikiwa wachezaji watano wa kimataifa na wachezaji watatu wawe wachezaji wa ndani.

Katika ripoti hiyo Robertinho ametaka golikipa, beki wa kushoto, beki wa kati, viungo wawili, winga mmoja na washumbuliaji wawili.

Katika mapendekezo yake, Mbrazil huyo katika wachezaji watano wapya wa kimataifa anaowataka (golikipa mmoja, beki wa kati mmoja, kiungo wa kati, winga na mshambuliaji mmoja).

Aidha, Robertinho ametaka wachezaji watatu wa ndani (ambao ni beki wa kushoto, kiungo wa kati na mshambuliaji mmoja).

Kwenye ripoti hiyo Robertinho anataka wachezaji wanaocheza timu zao za taifa na wawe kwenye kikosi cha kwanza kwenye timu wanazotoka.

Pia, kocha huyo amependekeza kuachana na wachezaji Mohamed Ouattara, Agustine Okrah, Peter Banda, Ismail Sawadogo, Gadiel Michael, Beno Kakolanya na Habibu Kyombo wakati Peter Banda akiomba kuondoka klabuni hapo kwa mkopo.

Katika hatua nyingine, kocha huyo ameomba wachezaji wawili wa kimataifa Pape Ousmane Sakho na Joash Onyango wasiondoke klabuni hapo, hii ni baada ya wachezaji hao kuomba kuondoka Simba SC.

Wachezaji wa kimataifa wenye uhakika wa kuendelea kubaki Simba kwa msimu ujao 2023/24 ni beki Henock Inonga Baka, viungo Sadio Kanoute, Clatous Chama na Saido Ntianzokiza na washambiaji Moses Phiri na Jean Baleke.

Pamoja na hayo, Robertinho ameomba kuongezewa watu kwenye bechi la ufundi ili kuifanya kuimarisha zaidi benchi la msimu huu.

SOMA NA HII  ACHANA NA STORY ZA VIJIWENI...ILE ISHU YA JOB KUTAKIWA MISRI..UKWELI WOTE HUU HAPA...