Home Ligi Kuu NAMUNGO: TUKO TAYARI KUUWASHA MOTO SHINYANGA

NAMUNGO: TUKO TAYARI KUUWASHA MOTO SHINYANGA

KIKOSI cha klabu ya Namungo kimetamba kujipanga vizuri kwa ajili ya kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mchezo wao wa leo dhidi ya Mwadui.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa katika dimba la Mwadui Complex, mkoani Shinyanga majira ya saa nane kamili mchana. 

Namungo wametamba kuwa, ushindi wa bao 1-0 walioupata siku ya Jumapili dhidi ya Mbeya City, katika michuano ya kombe la Shirikisho umezidi kuamsha ari ya kuhakikisha wanashinda mchezo wa leo. 

Akizungumzia maandalizi yao kuelekea mchezo huo, Ofisa habari wa Namungo, Kindama Namlia amesema: “Kikosi chetu kiliwasili salama mkoani Shinyanga jana kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wetu dhidi ya kikosi cha Mwadui.

“Ushindi tulioupata katika mchezo uliopita dhidi ya Mbeya City kwenye michuano ya kombe la FA, umezidi kutupa ari ya kufanya vizuri kwenye mchezo huu wa Ligi Kuu,”

SOMA NA HII  MZUNGUKO WA KWANZA WAKUSANYA MABAO 10 BONGO