Home Habari za michezo BOSI WA YANGA ASEMA HAYA KWA WALIWACHUKULIA POA KUWEKA KAMBI NCHINI

BOSI WA YANGA ASEMA HAYA KWA WALIWACHUKULIA POA KUWEKA KAMBI NCHINI

habari za yanga

Mtendaji Mkuu wa Yanga Andrew Mtine amewajibu wale wote waliokuwa wanachukulia poa timu ya Yanga kufanya Maandalizi yao ya Msimu ndani ya nchi na sio kwenda nje ya nchi.

Mtine amesema kikosi chao kiko imara ndiyo maana wameweza kupata ushindi kwa mara nyingine tena mbele ya Azam FC kwa kuwafunga bao 2-0 kwenye mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii pale Mkwakwani.

“Unaona wewe mwenyewe, nini ambacho Avic Town imekifanya kwetu? Imefanya vizuri sana, unaweza kuona fitness ya timu iko juu, muunganiko wa timu uko vizuri na kulikuwa na sababu kwa nini tulibaki hapa nchini, sababu ni kalenda.

“Kwenye soka sio suala la nani unamtaka, yeyote utakayepewa unatakiwa kupambana ili kupata ushindi. Sijipangii yeyote mimi nasema namna Yanga ilivyo yeyote yule tunacheza naye tu,” amesema Mtine.

Yanga sasa inasubiri mshindi wa mchezo wa leo kati ya Singoida Fountain Gate na Simba, ambaye atashinda watakutana kwenye fainali huku Azam akisubiri atakayeshindwa mchezo wa leo atakutana naye kwenye mchezo wa mshindi wa tatu.

SOMA NA HII  SAA CHACHE KABLA YA KUMALIZANA NA WAARABU LEO...MWAMNYETO ATOA HOFU YANGA....