Home Uncategorized KOCHA WA YANGA AZUIWA KURUDI TANZANIA NA MFALME WA UBELGIJI

KOCHA WA YANGA AZUIWA KURUDI TANZANIA NA MFALME WA UBELGIJI

KOCHA wa Yanga, Luc Eymael alitakiwa kurudi nchini leo Jumatano, akitokea kwao Ubelgiji alipokwenda kwa ajili ya masuala yake ya kifamilia ambayo aliyamaliza tangu wiki iliyopita lakini jambo hilo limeshindikana baada ya Mfalme wa Ubelgiji, Roi Philippe kuzuia
ndege zote za Kimataifa kutoka nchini humo.

Eymael anasema serekali ya Ubelgiji ilitoa tangazo rasmi kuwa hakuna mwananchi wake au raia yoyote aliyokuwa nchini humu kusafiri na ndege kwenda nchi nyingine yoyote kewani hakuna ndege yoyote ya Kimataifa ambayo itatua hapo kwao.

“Serekali walitoa tangazo la kuzuia ndege zote za Kimataifa kuja hapa kwetu Ubelgiji kwa maana hiyo suala langu la kuondoka na kufika hapo Jumatano kesho  limeshindikana kutokana na zuio hilo ambalo hatujafahamu mwisho wake lini ruhusa ya kusafiri itatoka,”

“Jambo hilo limefanyika na Serekali kutokana na maambukizi ya virusi vya corona kwa maana hiyo mpaka ugonjwa huu utapungua nadhani ndio ndege zitaanza kutua hapa kwetu na
kwenda nchini nyingine ingawa bado hatujafahamu itakuwa lini,
tunaendelea kusubiri.

“Sina jinsi na wala sina njia nyingine ya kurudi katika kituo changu cha kazi bila kutua usafiri wa ndege kwa maana hiyo naendelea kusubiri mpaka hapo serekali yetu itatangaza tena kufungua viwanja vyetu vya ndege na wananchi wake kutoka na wengine kuingia,” amesema Eymael.

SOMA NA HII  ZAHERA AMUWASHIA MOTO GADIEL MICHAEL, ATOA MASHARTI MAZITO KWA VIONGOZI YANGA