Home Uncategorized ZAHERA AMUWASHIA MOTO GADIEL MICHAEL, ATOA MASHARTI MAZITO KWA VIONGOZI YANGA

ZAHERA AMUWASHIA MOTO GADIEL MICHAEL, ATOA MASHARTI MAZITO KWA VIONGOZI YANGA


Kocha Mkuu wa Yanga Mkongomani, Mwinyi Zahera amesikia taarifa za beki wake wa pembeni, Gadiel Michael kugomea kusaini mkataba akasonya na kuwaambia viongozi; “Mnambembeleza wa nini?”

Hiyo, ikiwa ni siku chache tangu mmoja wa viongozi wa Yanga kusafiri na mkataba hadi nchini Misri inapofanyika Afcon kwa ajili ya kumsajili beki huyo aliyekuwa Taifa Stars iliyoondolewa katika michuano hiyo.

Beki huyo kwa mara ya pili amegomea kusaini mkataba baada ya hivi karibuni kukataa dau la Shilingi Milioni 50 alilowekewa mezani huku Simba ikielezwa kumuwekea 70 ambazo ameshawishika kusaini miaka mitatu Msimbazi.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, Zahera tayari amewaambia mabosi wa timu hiyo kuachana na mchezaji huyo kwavile si staa kiasi hicho wala gharama yake si kubwa kiivyo.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, kocha huyo tayari ametoa mapendekezo ya kumbakisha Haji Mwinyi aliyekuwa kwenye mipango ya kuachwa kwa ajili ya kusaidiana na Ally Mtoni ‘Sonso’.

Aliongeza kuwa, kocha anaamini kuwa wapo wachezaji wengine wenye uwezo mkubwa zaidi ya Gadiel, hivyo kuondoka kwake hakutamuumiza huku akimtakia kila heri huko aendako.

Habari zinasema Mwenyekiti wa timu hiyo, Mshindo Msolla ametoa mpaka kufikia leo Gadier kuelezea hatma yake kusaini Yanga kabla ya wao uongozi kufanya uamuzi.

SOMA NA HII  BAADHI YA PICHA YANGA WALIVYOTUPIA LEO MJENGONI DODOMA