Home Uncategorized MAKONDA ABEZWA JUU YA KUWAPA YANGA KIWANJA – VIDEO

MAKONDA ABEZWA JUU YA KUWAPA YANGA KIWANJA – VIDEO


MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema alibezwa na baadhi ya watu alipotangaza kuipa Yanga eneo.

“Wapo waliosema nawapa eneo la Manji (Yusuf aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga ambaye alitangaza kuwapa eneo Gezaulole).

“Kila mmoja aliongea lake, ilikuwa ni changamoto kubwa, lakini sasa nimekata mzizi wa fitina,” amesema Makonda leo wakati akikabidhi kiwanja hicho eneo la Kisarawe, Kigamboni.

Alisema ametoa eneo hilo la ekari saba sanjari na lile la ekari 15 kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokana na mahaba aliyonayo katika soka.

“Mimi ni shabiki wa Simba kindakindaki, lakini napenda maendeleo ya soka ndiyo sababu nimetoa maeneo hayo kwa Yanga na TFF,” alisema.

Alisema anatamani kuona sasa TFF na Yanga wanayaendeleza maeneo hayo ikiwezekana kujengwe kituo cha mfano ambacho kitazivutia timu za nje ya nchi kuweka kambi hapo.


SOMA NA HII  WANA KMC SASA WAANZA KUIVUTIA KASI MWADUI FC