Home Ligi Kuu SIMBA WAANGUKIA PUA MBEYA…YAPIGWA KIMOJA CHA UCHUNGU CHWAAA…PABLO ALAMBWA KADI YA NJANO…

SIMBA WAANGUKIA PUA MBEYA…YAPIGWA KIMOJA CHA UCHUNGU CHWAAA…PABLO ALAMBWA KADI YA NJANO…


Mpira umeisha katika Uwanja wa Sokoine ambapo Mbeya City imeibuka na ushindi mwembamba wa goli 1-0 dhidi ya Mabingwa wa Ligi Kuu Soka Tanzania bara Simba SC.

Ni Paul Nonga aliyepachika goli pekee la Mbeya City akitumia makosa ya mabeki wa Simba chini ya Inonga Banka.

Mpira uliaanza kwa kasi ambapo Simba kupitia kwa Chriss Mugalu walikuwa wa kwanza kuliona lango la Mbeya City lakkni goli hilo lilikataliwa na mwamuzi kwa kuwa lilikuwa la kuotea.

Hata hivyo  Mbeya City walikamilisha dakika 45 wakiwa pungufu kwa sababu nyota wao Mpoki Mwakinyuke alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 43.

Hata hivyo Simba wangeweza kubadili matokeo hayo na kuwa sare kama Chriss Mugalu angeweza kufunga Penati ambayo ilitokana na beki wa Mbeya City kuunawa mkono kwenye eneo la hatari.

Aidha, katika mchezo huo pia Kocha Mkuu wa Simba Franco Pablo alijikuta akipewa kadi ya njano na mwamuzi baada ya kumgasi mwamuzi wa akiba.

Kwa matokeo haya Simba SC imesalia na alama zake zilezile 24 katika nafasi ya pili nyuma ya Yanga, Wakati Mbeya City wakisogea mpaka nafasi ya tatu wakiwa na alama 19

SOMA NA HII  KISA SARE NA YANGA JANA...MGUNDA AIBUKA NA HAYA KWA WCHEZAJI SIMBA....