Home Uncategorized KAGERA SUGAR: TUTAPAMBANA KESHO KUPATA POINTI TATU ZA YANGA

KAGERA SUGAR: TUTAPAMBANA KESHO KUPATA POINTI TATU ZA YANGA


MECKY Maxime, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa watapambana kesho mbele ya Yanga uwanja wa Uhuru kupata matokeo mazuri.

Kagera Sugar itakutana na Yanga ikiwa na kumbukumbu ya kupokea kichapo cha mabao 2-1 mbele ya Polisi Tanzania kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Ushirika, Moshi.

Akizungumza na Saleh Jembe, Maxime amesema kuwa wanatambua ubora wa Yanga ulivyo ila watapambana kupata matokeo chanya kutokana na kuzihitaji pointi tatu.

“Hatujapata matokeo kwenye mechi yetu iliyopita ila kwa sasa tupo tayari kupambana na wapinzani wetu Yanga kwenye mechi yetu inayofuata, tunaachana na matokeo ya nyuma.

“Kwa sasa tupo Bongo tunajiaandaa na mchezo wetu muhimu dhidi ya Yanga, kikubwa ni kuona namna gani tunapata pointi tatu, kikubwa mashabiki watupe sapoti, ” amesema.

Kagera Sugar ipo nafasi ya nane kwenye ligi ikiwa na pointi 24 na Yanga ipo nafasi ya saba na ina pointi 25 ikiwa imecheza mechi 12 huku Kagera Sugar ikiwa imecheza mechi 16 za ligi.

SOMA NA HII  MUANGOLA WA YANGA SAFARI YA KUSEPA IMEWADIA