Home Habari za michezo HUKO SIO POA UNAAMBIWA NI KWA VITENDO SASA

HUKO SIO POA UNAAMBIWA NI KWA VITENDO SASA

eng

Hongera kwa Yanga SC kwa kufanikiwa kuchaguliwa katika tuzo za CAF katika kipengele Cha Timu Bora ya mwaka ni kweli wanastahili sababu katika msimu uliopita walifanikiwa kufika fainali maanake msimu ule walikusanya alama nyingi ambazo zimeiweka klabu katika nafasi nzuri pia imewasaidia kujulikana zaidi pamoja na wachezaji wengi kuvutiwa na Yanga.

Pili Pongezi kwa Benchi la Ufundi chini ya Nabi pamoja wachezaji na benchi la Ufundi kwa umoja na ushirikiano maanake mafanikio haya ni ushirikiano wa Hawa wote hasa wachezaji waliojitoa kwa Hali na Mali kuhakikisha wanapata mafanikio ndiyo maana hata mchezo wa marudiano dhidi ya Usm Alger walishinda na kutolewa kwa faida ya goli la ugenini.

Pia inaonesha ukubwa wa ligi yetu kwa Sasa tazama Mshambuliaji wa Zamani wa Yanga ambaye kwa Sasa anakipiga Pyramids Fiston Mayele amechaguliwa katika vipengele viwili kama mshambuliaji Bora wa Vilabu pamoja Mchezaji Bora wa mwaka wa Afrika pamoja kipa wa Yanga SC Djigui Diarra anawania Golikipa Bora pamoja na Mchezaji Bora wa Afrika kwa michuano ya klabu.

SOMA NA HII  NGOME MPYA YATENGENEZWA SIMBA