Home Habari za michezo AL AHLY AFL WATUPWA NJE YA MASHINDANO, WYDAD vs WYDAD KUKIPIGA FAINALI

AL AHLY AFL WATUPWA NJE YA MASHINDANO, WYDAD vs WYDAD KUKIPIGA FAINALI

African Football league

Mabingwa wa muda wote wa Ligi ya Mabingwa Afrika Klabu ya Al Ahly ya Misri wameondolewa kwenye michuano ya African Football League baada ya kutoa sare ya bila kufungana na Mamelodi Sundowns ya nchini Afrika Kusini.

Ikumbukwe kuwa katika mchezo wa kwanza uliopigwa wiki iliyopita, Mamelodi wakiwa nyumbani kwao, walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0, balo ambao limedumu mpaka kumalizika kwa mchezo wa leo na kuifanya Mamelodi itinge fainali.

Licha ya Ahly kupata penati dakika ya 8 tu mchezo kufuatia faulo aliyochezewa Percy Tau na kipa wa Mamelodi, Ronwen Williams lakini kipa huyo alipangua penati iliyopigwa na Al Maâloul dakika ya 12.

Dakika ya 84, Mamelodi walipata pigo jingine kwa mchezaji wao Junior Mendieta kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu mbaya mchezaji wa Ahly, Akram Tawfik lakini bado haikuwasaidia Waarabu kukwepa garika la Wasauzi.

Mamelodi itakutana katika fainali na Wydad Casablanca ya nchini Morocco ambayo imeiondoa Esperance ya Tunisia kwa changamoto ya mikwaju ya penati 5-4 baada ya kutoa sare ya 1-1 (matokeo ya jumla ya mchezo huo).

SOMA NA HII  WAKATI WENGINE WAKIPEWA 'THANK YOU'....YANGA NA SURE BOY MAMBO NI HIVI 🔥🔥🔥...