Home Habari za michezo UCHOCHORO WA SIMBA KUWA KIBONDE UKO HAPA

UCHOCHORO WA SIMBA KUWA KIBONDE UKO HAPA

Habari za Simba SC

Tangu Golikipia namba moja wa Simba SC, Aishi Manula apate majeraha ambayo ndiyo yamemweka nje mpaka sasa, Simba imekuwa sio timu tena ya kuhakikisha inalilinda lango lake kwa asilimia zote ili mpinzani asipate nafasi ya kuchafua Gazeti.

Hili linathibitishwa na takwimu za sasa ambazo zinaonesha kwamba Timu hiyo katika mechezo yao mitatu ya mwisho ukijumlisha na wa juzi dhidi ya Power Dynamos wameruhusu magoli 5 na mchezo pekee ambao hawakuruhusu goli ni dhidi ya Dodoma Jiji pekee.

Takwimu za Simba katika mechi nne za mwisho

Simba SC v Ziré (1-1)❌

Mtibwa Sugar v Simba SC (4-2)❌

Simba SC v Dodoma Jiji (2-0) ✅

Power Dynamo’s v Simba (2-2)❌

Mechi – 4

Cleansheet – 1.

SOMA NA HII  LIGI YA MABINGWA AFRIKA KWA WANAWAKE KUANZA KATI YA OKTOBA NA NOVEMBA