Home Habari za michezo ROBERTINHO AKUNA KICHWA AONA HAPANA……….. SASA AMEKUJA NA HESABU HIZI

ROBERTINHO AKUNA KICHWA AONA HAPANA……….. SASA AMEKUJA NA HESABU HIZI

Habari za Simba

Kocha wa Simba, Robert Olveira ‘Robertinho’ amesema wanarudi na hesabu kali huku wakijipanga vizuri kwa kushinda watakapokuwa nyumbani mbele ya mashabiki wao, lakini kwanza wanatakiwa kujipanga kupunguza makosa yaliyowagharimu ugenini.

“Tumecheza vizuri, ingawa tulikuwa na baadhi ya makosa ambayo yaliwapa nafasi wapinzani wetu, nilisema kabla hii timu ni nzuri (Power Dynamos) lakini bado nafasi yetu ni kubwa tutarudi imara zaidi tutakapokuwa nyumbani,” alisema Robertinho na kuongeza;

“Tutakwenda kufanyia kazi changamoto ambazo tumekutana nazo juzi Simba ni timu kubwa itatengeneza ushindi mkubwa tukiwa mbele ya mashabiki wetu.

SOMA NA HII  WAKATI SIMBA , YANGA WAKIENDELEA KUTANGAZA WACHEZAJI WAKE WAPYA.... WASENEGAL WA AZAM WATAMBA TUNISIA