Home Uncategorized YANGA NA AZAM FC ZINADAIWA MABAO ZAIDI YA 10 NA SIMBA

YANGA NA AZAM FC ZINADAIWA MABAO ZAIDI YA 10 NA SIMBA


 SAFU ya ushambuliaji ya Simba inayoongozwa na mzawa John Bocco imekuwa bora kwa msimu wa 2020/21 huku ikizipoteza zile za wapinzani wao Azam FC inayoongozwa na Prince Dube yenye mabao 18 na ile ya Yanga inayoongozwa na Michael Sarpong yenye mabao 13.

Rekodi zinaonyesha kwamba licha ya Simba kuwa nafasi ya tatu,inamiliki vinara wote wa rekodi kwa msimu wa 2020/21 ikiwa ni kwenye safu ya ushambuliaji na vinara wa pasi za mwisho.

Idadi ya mabao ni mtaji mkubwa kwa Simba hapo baadaye ikiwa itatokea zitagongana pointi kama ilivyo kwa Yanga na Azam ambapo zote zina pointi sawa ila Azam faida ya mabao mengi imeipa nafasi ya kuwa ya kwanza.

Kinara wa utupiaji ni Bocco mwenye mabao saba na pasi moja ya bao huku kinara wa pasi za mwisho ni Luis Miquissone mwenye pasi sita na bao moja. Huku Yanga wakiwa ni vinara kwenye safu imara ya ulinzi ikiwa imeruhusu mabao matano na haijapoteza.



Simba imecheza  mechi 11 na imefunga jumla ya mabao 29 ipo nafasi ya tatu na pointi zake 23 ina wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 34 watani zao wa jadi Yanga wakiwa nafasi ya pili na pointi 25 mechi 11 safu yao ya ushambuliaji imekusanya mabao 13 ikiwa inadaiwa mabao 16 ili kuifika yale ya Simba.

Safu ya ushambuliaji ya Yanga ina wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 76 kwenye mechi za ligi. Azam FC ambao ni vinara wakiwa na pointi 25 kwenye mechi 11 ambazo ni dakika 990, safu yao ya ushambuliaji imefunga mabao 18 ina wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 55 inadaiwa mabao 11 ili kuwafikia mabingwa watetezi Simba.



Sven Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba ameliambia amesema kuwa kufunga ni kazi ya wachezaji wake ili kupata ushindi huku Cedric Kaze Kocha Mkuu wa Yanga ameweka wazi kuwa kuna tatizo kwenye safu yake ya ushambuliaji na Vivien Bahati kocha msaidizi wa Azam FC ameweka wazi kuwa hesabu zao ni pointi tatu bila kujali idadi ya mabao.

SOMA NA HII  SAMATTA KUTUA LIGI KUU ENGLAND AMEACHA DENI KUBWA