Home Habari za Usajili Yanga YANGA YAMFICHA AGEE AVIC…ANA BALAA ZITO…INJINIA HERSI AMALIZA MAMBO

YANGA YAMFICHA AGEE AVIC…ANA BALAA ZITO…INJINIA HERSI AMALIZA MAMBO

HABARI ZA YANGA LEO

YANGA bado inapiga hesabu za kusajili winga wa maana na mezani kwao kuna mawinga wawili akiwemo Philipe Kunzumbi na Basiala Agee, lakini mmoja kati ya hao wawili akawahishwa kambi ya klabu hiyo ya Jangwani iliyopo Avic Town fasta akiwekewa mtego wa maana.

Yanga ilimfungia safari Agee baada ya Rais wa klabu hiyo, Injinia Hersi Said kumsoma winga huyo kwa macho wakati timu anayoichezea ya AS Union Maniema ikicheza dhidi ya FC Lupopo.

Katika safari hiyo inaelezwa kwamba, Injini Hersi alimpatia mcheaji huyo mkataba wa awali, huku kila kitu wakisubiri kukamilisha Ligi itakapomalizika mbappo tayari kila kitu kipo wazi.

Winga huyo inaelezwa kwamba tayari kishatua bongo na yupo mitaa ya Avic Town anasubiriwa kutambulishwa tu.

Kama ambavyo tuliripoti mapema Januari kwamba Basiala Agee ameshasinya mkataba na kilihobaki ni kutua nchini. Seehmu ya Ripoti yetu iliandika hivi;

Taarifa za uhakika zinasema kuwa Yanga imeshatuma mkataba huo na winga huyo atatakiwa kuusaini ndani ya wiki hii na baadaye atatumiwa tiketi ili kuja kujiunga na Wanajangwani hao.

Yanga tayari ilishakubaliana kila kitu na tajiri wa Maniema, Jenerali wa jeshi wa timu hiyo, Amissi Kumba na hatua ya Basiala kusaini sasa inakwenda kuwa uhakika kuwa winga huyo ni mali ya Yanga.

“Yanga wameshatuma mkataba upande wa mchezaji watausoma na kuangalia mambo ya kuweka sawa huku kwa klabu kila kitu kilishamalizika kupitia jenerali (Amissi Kumba),” alisema bosi mmoja wa Maniema.

“Wakimalizana watamtumia tiketi, ili aje lini huko Tanzania, hayo yatakuwa mambo yao kati ya Yanga na mchezaji, wanajua wanafanya njia gani taratibu zao, nafikiri hizi siku mbili Agee atasaini na kuja Tanzania.

SOMA NA HII  MSHERY NA KHOMEIN WAJIPANGE SANA KWA DIARRA