Home Habari za Usajili Yanga YANGA MWENDO WA DOZI TU…SASA KUKIPIGA NA TIMU YA BUNDASLIGA

YANGA MWENDO WA DOZI TU…SASA KUKIPIGA NA TIMU YA BUNDASLIGA

habari za yanga

Kabla ya kuikabili Kaizer Chiefs katika mchezo wa Toyota Cup utakaopigwa Julai 28, Wananchi Yanga watakuwa Afrika Kusini mapema kushiriki michuano mingine waliyoalikwa, Mpumalanga Premier International Cup.

Kulingana na ratiba ya michuano hiyo ambayo itarushwa mbashara na kituo cha televisheni cha SABC 1, Julai 20 Yanga itachuana na FC Augsburg ya ligi kuu ya Ujerumani wakati Ts Galaxy wakichuana na Mbabane Swallows.

Mchezo utakaofuata kwa Yanga ni Toyota Cup Julai 28 dhidi ya wenyeji wao Kaizer Chiefs.

Yanga pia ina mialiko kutoka Kenya na Rwanda, pengine itacheza mechi nyingine kabla ya kuhitimisha maandalizi ya msimu mpya kwa mchezo wa kilele cha wiki ya Mwananchi August 04.

Msimu huu Yanga itakuwa na pre-season bora zaidi pengine kuliko wakati mwingine wowote katika misimu ya karibuni.

Lakini pia Yanga kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika wana kazi ya kusaka ushindi dhidi ya Vital’O ya Burundi kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali.

Baada ya droo kuchezwa nchini Misiri Julai 11 2024, Yanga itaanzia ugenini kusaka ushindi kwenye mchezo wa kimataifa.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kati ya Agosti 16-18 marudiano Bongo itakuwa kati ya Agosti 23-25.

Vijana hao wa mitaa ya Jangwani wataanzia ugenini kwenye mchezo ambao utachezwa kati ya Agosti 16-18, 2024 na kurudiana kati ya Agosti 23-25.

Klabu ya Yanga imesajili wachezaji kibao wenye majina mkubwa na uwezo uwanjani,  kuna Clatous Chama, Prince Dube, Chadrack Boka, Aziz Andabwile, na sasa Duke Abuya.

Wachezaji wanaohusishwa zaidi kujiunga na Simba, ni Jean BALEKE aliyewahi kucheza Simba kwa msimu mmoja na nusu akifunga jumla  ya mabao 16, kisha akatimkia kwenda klabu ya Al Ittihad ya Libya.

SOMA NA HII  YANGA WAENDELEA KUKISUKA UPYA KIKOSI CHAO KIMYA KIMYA...KIFAA KIPYA KUTOKA BURUNDI HIKI HAPA....