Home Uncategorized ROSE MUHANDO MAJANGA TENA

ROSE MUHANDO MAJANGA TENA


LICHA ya hivi karibuni kusaidiwa na baadhi ya waimbaji wa Injili wa nchini Kenya alipokuwa anaumwa, habari za ndani zinadai kwamba kwa sasa muimbaji wa Injili Bongo, Rose Muhando ameharibu tena nchini humo kutokana na kutapeli baada ya kupewa fedha kwa ajili ya uimbaji, lakini hakutokea eneo la tukio. 

Chanzo makini kilidai kwamba, baada ya Rose kupona, watu mbalimbali walimpa fedha ili akatoe huduma ya uimbaji nchini Kenya, lakini hakwenda na hadi sasa wanamsaka.

“Yaani Rose bado ni tatizo, ametapeli tena Kenya hivyo kutokana na hilo watu hao wamepeleka mashtaka dhidi yake kwenye Chama cha Muziki wa Injili hapa Bongo ili kiwasaidie kumpata akafanye kazi kama walivyokubaliana,” kilisema chanzo hicho.

CHAMA KINASEMAJE?

Kutokana na kupata habari hizo kutoka kwa chanzo, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Katibu wa Chama cha Muziki wa Injili cha Tanzania Music Foundation (TAMUFO), Stella Joel ambaye alikiri kupokea malalamiko hayo kutoka nchini Kenya.

“Ni kweli tumepata malalamiko ya Rose kuchukua fedha kwa watu huko Kenya kwa ajili ya huduma, lakini hakwenda kufanya, lakini hatuwezi kuzungumzia sana, tumemwita ili tuzungumze naye na akishatoa maelezo kuhusiana na hilo ndipo tutakapotoa ufafanuzi zaidi,” alisema Stella.

Ili kupata mzani wa habari hii, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Rose kwa njia ya simu ili azungumzie tuhuma hizo, lakini simu yake haikuwa hewani.

Alipotafutwa meneja wake, Nathan kwa njia ya Mtandao wa WhatsApp na kusomewa mashtaka ya msanii wake huyo, alisoma madai hayo na hakujibu chochote. Mara kadhaa Rose amekuwa akikumbwa na skendo za utapeli kiasi cha kuomba radhi na kila mtu kujua amebadilika hivyo kuibuka kwa madai hayo kunamjengea taswira nyingine

SOMA NA HII  HIKI HAPA KILIMPOTEZA MUUAJI WA YANGA JUMLA KWENYE LIGI