Home Habari za Simba Leo SIMBA YAPIGA HODI KWA KAPUMBU…KIBOKO YA YANGA.

SIMBA YAPIGA HODI KWA KAPUMBU…KIBOKO YA YANGA.

HABARI ZA SIMBA

MBONA mtakoma msimu huu, Baada ya kumalizana na winga Joshua Mutale (22), mabosi wa Simba wamedaiwa hawajamaliza kazi huko Zambia baada ya kuhamia kwa kiungo mkabaji wa Zesco United, Kelvin Kapumbu (28) kwa nia ya kumvuta Msimbazi kukiwasha kwa msimu ujao wa mashindano ya ndani na yale ya kimataifa.

Hata hivyo, taarifa hizo kutoka ndani ya Simba zinasema kuwa mabosi wa klabu hiyo hasa wanaosimamia usajili wamegawanyika juu ya umri wa chezaji huyo, japo walio wengi wanapendekeza aletwe hata kwa mkataba wa muda mfupi kwani ana kitu kitakachoibeba timu hiyo katika Kombe la Shirikisho Afrika.

Inalezwa kwamba Muwekezaji wa Simba MO Dewji yeye anahitaji wachezaji watakao sajiliwa klabuni hapo, wawe na umri mdogo ili kuendana na kasi ya mchezo kwa sasa.

Pia faida ya mchezaji mwenye umri mdogo kwa Simba ni kuwa na uhakika wa kumtumia hata kwa misimu 4, kutoka na umri kuruhusu, na hii itawafanya wao kufikia malengo waliyojiwekea baada ya kupotea kwa misimu mitatu.

Kama mambo yataenda sawa, Kelvin Kapumbu atavaa jezi ya Simba msimu ujao, ikumbukwe ya kwamba miamba hii imekua na bahati sana na wachezaji wa Kizambia kwa miaka mingi.

Ujio wa Kapumbu utaongeza kitu cha tofauti kwenye eneo la kiungo ambalo msimu uliomalizika halikufanya maajabu mengi, kama usajili wa mchezaji huyu utakamilika, basi hakutakuwa na umuhimu tena wa Saidoo Ntibazonkiza ambaye umri wake umeenda sana.

SOMA NA HII  LEONEL ATEBA APANDISHA MZUKA…ANATAKA MAKOMBE SIMBA