Home Yanga SC YANGA KUFANYA MABADILIKO MAKUBWA KWENYE KIKOSI

YANGA KUFANYA MABADILIKO MAKUBWA KWENYE KIKOSI


 KAIMU Kocha Mkuu wa Yanga, Juma Mwambusi, Jumamosi iliyopita aliiongoza timu hiyo kwa mara ya kwanza kwenye Ligi Kuu Bara baada ya kukabidhiwa mikoba, akaambulia sare ya 1-1 dhidi ya KMC.

 

Sasa baada ya mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar, Mwambusi amesema atafanya mabadiliko makubwa ya kikosi chake katika mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United utakaochezwa kesho, uwanjani hapo.

 

Mwambusi ambaye anaiongoza Yanga baada ya Kocha Cedric Kaze kutimuliwa Machi 7, mwaka huu, amezitaja sehemu ambazo zimeonekana kuwa na matatizo sugu kwamba ni safu ya ulinzi na ushambuliaji.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Mwambusi alisema: “Baada ya kupata sare na KMC, kikosi kinaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Biashara United.


“Tunafahamu kwamba tunapaswa kufanya vizuri katika mchezo huo ili tupate ushindi na kurejesha hali ya kujiamini na ushindani katika kuelekea kufikia malengo ya kuwa mabingwa.

 

“Kuelekea mchezo dhidi ya Biashara, tutaendelea kuona mabadiliko katika nafasi kadhaa ndani ya uwanja, ikiwemo kwenye safu ya ushambuliaji na ulinzi kama ambavyo tuliona dhidi ya KMC ambapo Abdallah Shaibu ‘Ninja’ alianza.

 

“Tunafanya hivi ili kuona tunapata uwiano mzuri wa matumizi ya wachezaji wetu na kupunguza makosa yetu, ili kuhakikisha tunamaliza kiu ya mashabiki wetu ya kukosa ushindi kwa muda,” .

SOMA NA HII  BAADA YA KUIONA YANGA INAVYOCHEZA...JEMBE LA TP MAZEMBE..LATIKISA KICHWA KISHA ATEMA CHECHE HIZI...