Home Simba SC SIMBA YAPELEKWA FIFA KISA MADAI YA MKWANJA

SIMBA YAPELEKWA FIFA KISA MADAI YA MKWANJA


 INAELEZWA kuwa aliyekuwa kocha mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amepeleka malalamiko yake ya madai ya stahiki zake kwenye Shirikisho la Soka Duniani, (FIFA).

 Vandenbroeck ameipeleka Simba FIFA kudai malipo ya dola za Marekani 44,000 zaidi ya millioni 100 za kibongo, ambazo anadai ni malipo ya bonasi.


Inaripotiwa baada ya muda mrefu kuomba alipwe stahiki zake, mambo yalikuwa tofauti na alivyoahidiwa sasa amepeleka malalamiko yake FIFA.

Suala hili lilipelekwa FIFA wiki zilizopita na Shirikisho hilo la soka limethibitisha kuanza kulifanyia kazi shauri hilo.


Vandenbroeck alikiongoza kikosi cha Simba kutinga hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na alisepa baada ya kufanikisha malengo hayo ya Simba.
Kwa sasa kikosi hicho kipo mikononi mwa Didier Gomes ambaye amekifikisha kikosi hicho hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
SOMA NA HII  KISA KOSA KOSA ZA KINA KAGERE,....KOCHA SIMBA KAAMUA KUWATOLEA UVIVU...AFUNGUKA WALICHOFANYIWA...