Home Uncategorized ALIYENYOOSHWA NA MWAKINYO TINAMPAY KUKUTANA NA MUZIKI WA MFAUME

ALIYENYOOSHWA NA MWAKINYO TINAMPAY KUKUTANA NA MUZIKI WA MFAUME


PROMOTA wa mapambano ya ngumi nchini Juma Msangi maarufu kama Jay Msangi amesema kuwa bondia Mfaume mfaume amesaini mkataba wa kuzichapa na bondia Arnel Tinampay kutoka nchini Thailand.
Tinampay Novemba 2019 alizichapa na bondia Hassan Mwakinyo  ambapo katika pambano hilo alipoteza kwa pointi katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar.
Msangi amesema kuwa tayari bondia mfaume ameshasaini mktaba wa kupigana na bondia huyo hivyo hivi karibuni watatangaza tarehe na mahali pambano litakapofanyika kutokana na kusubiri kibali cha Serikali.
“Kwa sasa tunasubiri kibali cha Serikali kuturuhusu kwa ajili ya mapambano ya ngumi,lakini kuhusu mpambano huo tayari bondia Mfaume ameshasaini mkataba wa kupigana hivyo mambo yakiwa sawa tutangaza mpambano utafanyika lini na sehemu gani,”amesema Msangi.

SOMA NA HII  MTIBWA SUGAR INA KAZI KWENYE SAFU YA ULINZI, KOCHA HANA MASHAKA