Home Habari za michezo NTIBAZONKIZA AFUNGUKA KILICHOMFANYA AENDELEE KUBAKI KATIKA KLABU YA SIMBA

NTIBAZONKIZA AFUNGUKA KILICHOMFANYA AENDELEE KUBAKI KATIKA KLABU YA SIMBA

Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Burundi na Klabu ya Simba SC Saido Ntibazonkiza, amesema amerejea kivingine kwenye majukumu yake ndani ya klabu hiyo kuelekea msimu wa 2023/24.

Ntibazonkiza alimaliza msimu uliopita akiwa na mabao 17 sawa na Fiston Mayele wa Young Africans, hivyo wote wakatunukiwa kiatu cha ufungaji bora msimu wa 2022/23.

Akizungumza jijini Dar es salaam kabla ya kuanza safari ya kuelekea Uturuki, Ntibazonkiza amesema sasa likizo imeisha na amerejea kazini kivingine kuhakikisha wanaungana na wachezaji wenzake kufikia malengo ya klabu.

Amesema anaimani msimu huu watakuwa bora zaidi ya msimu uliopita kwa sababu ya maboresho ya kikosi cha timu yao na kuamini watafanya vizuri zaidi na kufikia kile ambacho kinatarajiwa na Wanasimba.

“Likizo imekwisha na nimerejea kazini katika majukumu yetu kwenda kufikia malengo ambayo tunayahitaji ikiwamo kutwaa mataji yote ya mashindano ya ndani na kufanya vizuri zaidi kwenye michuano ya kimataifa,” amesema.

Amesema anaamini viongozi wamefanya usajili kulingana na mahitaji ya timu yao, hivyo kwa kushirikiana na wachezaji wenzake wanatarajia malengo hayo ya msimu ujao kufanikisha malengo yanayokusudiwa.

SOMA NA HII  ROBERTINHO ANOGESHA USAJILI WA SIMBA AJA NA MDAKA RISASI KUTOKA BRAZILI...... HUKU SABABU ZAKUWEKA KAMBI UTURUKI ZATAJWA