Home news BAADA YA KUIONA YANGA INAVYOCHEZA…JEMBE LA TP MAZEMBE..LATIKISA KICHWA KISHA ATEMA CHECHE...

BAADA YA KUIONA YANGA INAVYOCHEZA…JEMBE LA TP MAZEMBE..LATIKISA KICHWA KISHA ATEMA CHECHE HIZI…


JEMBE jipya la Yanga, Chico Ushindi amefunguka kuhitaji kutengeneza nafasi nyingi za mabao ambazo pindi atakapoanza kuitumikia rasmi Yanga ambazo zitawafanya mastraika wa timu hiyo wakiongozwa na Fiston Mayele na Heritier Makambo kufunga mabao ya kutosha.

Ushindi ambaye anamudu kucheza winga zote ni usajili mpya kwa Yanga ambaye amesajiliwa kwa mkopo akitokea katika Klabu ya TP Mazembe ya nchini DR Congo.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Ushindi aliweka wazi kuhitaji kutengeneza nafasi nyingi za kufunga kwa washambuliaji wa timu hiyo pindi atakapoanza kuitumikia rasmi Yanga katika michezo mbalimbali ambayo wanashiriki msimu huu.

“Yanga tayari nimeshaona jinsi ambavyo wanacheza, ni timu ambayo inatumia sana wachezaji wa pembeni katika kutengeneza nafasi za kufunga. Mimi pia nacheza huko hivyo naona nafasi ya kutengeneza zaidi nafasi za kufunga kwa washambuliaji wa kati.

“Kusajiliwa na kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza mara kwa mara ni jambo jingine, hivyo ngoja tuone itakuwaje lakini nahitaji kucheza ili kuweza kuisaidia Yanga kufanya vizuri pamoja na kubeba ubingwa wa ligi kuu,” alisema winga huyo.

SOMA NA HII  RASMI....MSUVA HUYOOO MBEYA CITY....MAMBO YOTE YAKO HIVI 🔥🔥🔥🔥....