Home EURO 2020 ITALIA YATINGA NUSU FAINALI EURO 2020

ITALIA YATINGA NUSU FAINALI EURO 2020


TIMU ya taifa ya Italia imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali katika Euro 2020 kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ubelgiji katika mchezo wa robo fainali.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Allianz Arena kazi ilikamilika kipindi cha kwanza kwa kuwa mabao yote matatu yalifungwa wakati huo.

Alikuwa ni Nicolo Barella ambaye alifungua pazia la mabao dk ya 31 na msumari wa pili ambao ulikuwa ni wa ushindi ulipachikwa na Lorenzo Insigne dk ya 44 huku lile la Ubelgiji likipachikwa kimiani na   Romelu Lukaku dk 45+2 kwa mkwaju wa penalti.



Ushindi huo unaifanya Italia kusonga mbele hatua ya nusu fainali ambapo inatarajiwa kukutana na Hispania Uwanja wa Wembley kwenye mchezo wa nusu fainali huku Ubelgiji ambao walikuwa wanapewa nafasi ya kushinda wakiwa hawaamini namna walivyopoteza bahati ya dhahabu.

SOMA NA HII  MICAH RICHARDS AIONYA ENGLAND MBELE YA ITALY