Home Habari za michezo DUUH! CHEKI JUMBA HILI LA KIFAHARI LA RONALDO…LAPANGISHWA MAMILIONI KWA MWEZI

DUUH! CHEKI JUMBA HILI LA KIFAHARI LA RONALDO…LAPANGISHWA MAMILIONI KWA MWEZI

DUUH! CHEKI JUMBA HILI LA KIFAHARI LA RONALDO...LAPANGISHWA MAMILIONI KWA MWEZI

Nyota wa klabu ya Alnassr na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo ameripotiwa kuwa anakodisha/pangisha jumba lake la Kifahari lililopo katika jiji la Madrid nchini Unispania kwa euro 10,000 tu (takriban $10,980) sawa na Tsha 25,726,140/= (Milioni 25 za Kitanzania) kwa mwezi!

Jumba hilo lenye ukubwa wa mita za mraba 43,000 linaelezwa kuwa lina vyumba saba vya kulala, bafu tisa, mabwawa mawili ya kuogelea, (Swimming Pool) uwanja wa mpira wa miguu, na kituo cha mazoezi ya viungo vya hali ya juu (Gym) na baadhi ya miongoni mwa maeneo mengine ya kifahari kama chumba cha Cinema na mengine.

Jumba hilo la Kifahari la Ronaldo linaelezwa kuwa ni miongoni mwa majumba ya Kifahari zaidi huku likiwa na paking ya magari ya ndani.

Kupitia mtandao wa @archdaily watu wengi wameweka comment zao wakidai kiasi hicho ni kidogo sawa kutokana na namna jumba hilo la Ronaldo lilivyofafanuliwa ukubwa wake.

SOMA NA HII  SAMATTA AWATAMBIA WA NIGER KUWANIA TIKETI YA KOMBE LA DUNIA