Home Habari za michezo HATIMA YA AISHI MANULA…KUAMULIWA LEO SIMBA…ISHU NZIMA IKO HIVI

HATIMA YA AISHI MANULA…KUAMULIWA LEO SIMBA…ISHU NZIMA IKO HIVI

HATIMA YA AISHI MANULA...KUAMULIWA LEO SIMBA...ISHU NZIMA IKO HIVI

Kipa namba moja wa Simba, Aishi Salum Manula leo atakutana na jopo la matabibu wa timu kutazamwa hali yake ili kujua kama yuko tayari kuanza mazoezi kuelekea mchezo dhidi ya Wydad Casablanca.

Simba watamenyana na Wydad Casablanca Jumamosi katika mechi ya kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Aishi alikosekana kwenye mechi mbili zilizopita za Ligi Kuu ya nyumbani dhidi ya Ihefu huko Mbarali Aprili 10 na Yanga jana, baada ya kuumia kwenye Azam Sports Federation Cup Aprili 7 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Lakini Afisa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally amesema kikosi kinaanza mazoezi leo Uwanja wa Mo Simba Arena baada ya mapumziko ya siku moja ya jana kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi ya mtani, Yanga kwenye Ligi Kuu Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Kipa namba mbili pia, Beno Kakolanya anatarajiwa kuwa tayari kwa mechi hizo mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika, ukwemo na ule Aprili 28 Casablanca baada ya yeye pia kukosekana kwenye mechi zote mbili hizo zilizopita kwa sababu ya majeruhi pia.

SOMA NA HII  BAADA YA MORRISON KUMTAJA KUWA ANAMFUNDISHA LUGHA YENYE MATUSI...MKUDE AIBUKA NA KUMJIBU HAYA...