Home Uncategorized ISHU YA KESI YA MKATABA WA MORRISON UONGOZI WA SIMBA WATOA UFAFANUZI,...

ISHU YA KESI YA MKATABA WA MORRISON UONGOZI WA SIMBA WATOA UFAFANUZI, WAITAJA YANGA

 UONGOZI wa Simba umesema kuwa kuhusu suala la Bernard Morrison kutangazwa ndani ya Simba ilihali ana kesi ya kimkataba lazima ianze kwenye mkataba wa awali na hakukuwa anayewazuia kumtambulisha.


Simba imemtambulisha Morriosn ambaye alikuwa na mvutano mkubwa ndani ya Yanga kuhusu masuala ya mkataba ambapoYanga walikuwa wanasema kuwa ana dili la miaka miwili huku Morrison akisema kuwa mchezaji alikuwa na miezi sita.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema hivi:“Kesi ya kimkataba inauhisiano gani na Morrison kusajiliwa, mchezaji kafika tarehhe 17 wao wanasema wamemsajili tarehe 15 inaoneshwa kwamba mkataba wa kwanza umesajiliwa tarehe 15, Yanga wamemuingiza kwenye mkataba tarehe 15 sasa kwahiyo hapo wajadili suala la mkataba wa kwanza.

“Waache kutuchezea mambo ya ajabu, tarehe 15 dirisha dogo la usajili lilifungwa, Morrison alitua nchini tarehe 17 sasa hapo anzeni pale, kuna mkataba ambao umesainiwa kwenye page nne sasa mkataba wa Morriosn una page moja kwa nini?

“Kamati ya hadhi ya wachezaji haiwezi kufanya mambo ya ajabuajabu, cha kwanza kiangaliwe mkataba wa kwanza kama ni halali ama sio halali, hivyo amecheza mechi za Singida na Tanzania Prisons akiwa hana mkataba, mkataba wake unaonyesha kwamba amesajiliwa kabla ya muda,” amesema.

Chanzo:Wasafi FM

SOMA NA HII  NDEMLA AIMALIZA ALLIANCE KWA KUKAMILISHA 5G TAIFA