Home Michezo KUMBE YANGA WALIFANYA HAYA KUIFUNGA SIMBA…KIBADENI ANYOOSHA MIKONO JUU

KUMBE YANGA WALIFANYA HAYA KUIFUNGA SIMBA…KIBADENI ANYOOSHA MIKONO JUU

KUMBE YANGA WALIFANYA HAYA KUIFUNGA SIMBA...KIBADENI ANYOOSHA MIKO JUU

NJAA YA MAFANIKIO
Yanga ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara na ndiyo mabingwa wa kihistoria wa taji hilo waliloshinda mara 29, Simba yenyewe imelichukua mara 22.

Ally Kamwe ambaye ni Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, amebainisha msimu huu malengo yao ni kutetea mataji yao, hivyo wanazicheza mechi zao kwa ajili ya kufanikisha jambo hilo.

“Tunahitaji kufikia malengo yetu ya msimu huu ambayo ni kutetea ubingwa, hatuwezi kutetea ubingwa kama tukidondosha ovyo pointi, lazima tushinde mechi zote zilizo mbele yetu bila ya kuangalia mpinzani gani tunakutana naye,” alisema Kamwe.

UPAMBANAJI
Kutokana na ishu hiyo ya njaa ya mafanikio, ndiyo inatoa taswira ya upambanaji kwa wachezaji wa Yanga kila wanaposhuka dimbani.

Ndani ya kikosi cha Yanga, safu yao ya ulinzi inaongoza kwa kuwa na ukuta mgumu sana kupitika, lakini pia ushambuliaji moto unawashwa si kitoto.
Timu hiyo ikiwa imeruhusu mabao 11 katika mechi 21, wakati wapinzani wao Simba, wakiruhusu 19 baada ya mechi 20.

Yanga wapo vizuri katika kucheka na nyavu, wachezaji wake tofauti wana mabao mengi na Stephane Aziz Ki amefunga 14, Maxi Nzengeli (9), Mudathir Yahya (8) na PacĂ´me Zouzoua (7). Hao ni wale wanaofuatana kwa ukaribu sana.

Yanga katika ishu ya kufunga mabao, ina wastani wa kufunga mabao (3) kila mechi, huku Aziz Ki ndiye kinara, wakati Simba wastani wao wa kufunga bao kila mechi ukiwa ni (2), kinara wao ni Saidi Ntibazonkiza na Clatous Chama ambao kila mmoja anayo 7.

Katika mechi 21 walizocheza Yanga, wameshinda 18, ndiyo timu iliyoshinda mechi nyingi zaidi ya zote zinazoshiriki ligi hiyo. Pia ina sare 1 na kupoteza mbili.

KUTOMTEGEMEA MTU MMOJA
Kwa namna kikosi cha Yanga kilivyo hivi sasa, Kocha Miguel Gamondi ametengeneza kitu kinachowafanya wasiwe wanamtegemea mtu mmoja kuwapa matokeo chanya kwenye mechi zao.

Wakati mwingine anaweza kukosekana mchezaji muhimu wa kikosi cha kwanza, lakini akaibuliwa yule anayekaa benchi sana au asiyepata nafasi kabisa, akaja kuwashangaza.

Tumeshuhudia hiyo kwenye mechi mbili za robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu walipocheza dhidi ya Mamelodi Sundowns ambapo Yanga iliwakosa Pacome Zouzoua, Yao Attohoula na Khalid Aucho.

Licha ya Yanga haikufanikiwa kusonga mbele kwenye michuano hiyo kutokana na kuondolewa kwa penalti 3-2, baada ya mechi zote kumalizika kwa matokeo ya 0-0, lakini hakuna kilichoharibika ndani ya uwanja.

Jonas Mkude alicheza eneo la kiungo mkabaji anapocheza Khalid Aucho na kufanya vizuri akishirikiana na Mudathir Yahya. Kule kwa Yao, alikuwepo Dickson Job ambaye mara nyingi hukucheza beki wa kati, pia ana uwezo wa kucheza beki wa kulia anapocheza Yao.

Kuhusu hilo, aliyewahi kuwa mchezaji na kocha wa Simba, Abdallah Kibadeni, amesema:

“Yanga msimu huu wana kikosi kilichokamilika, ukiangalia hivi karibuni wamecheza mechi mbili dhidi ya Mamelodi katika michuano ya kimataifa bila ya wachezaji wao muhimu, lakini kila mmoja ameona nini kilitokea, ndiyo maana nasema Yanga wamekamilika, wana kikosi ambacho akikosekana mtu fulani, inakuwa kama vile hakijatokea kitu.”

SOMA NA HII  KISA KOSA KOSA ZA KINA KAGERE,....KOCHA SIMBA KAAMUA KUWATOLEA UVIVU...AFUNGUKA WALICHOFANYIWA...