Home epl LIVERPOOL WAFUFUA MATUMAINI KUMALIZA NDANI YA NNE BORA

LIVERPOOL WAFUFUA MATUMAINI KUMALIZA NDANI YA NNE BORA


 LIVERPOOL inayonolewa na Kocha Mkuu, Jurgen Klopp ikiwa ugenini usiku wa kuamkia leo imesepa na pointi tatu muhimu mbele ya Burnley jambo linalowapa matumaini ya kuweza kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Baada ya dakika 90 kukamilika ubao wa Uwanja wa  Turf Moor ulisoma Burney 0-3 Liverpool jambo ambalo linawapa nafasi mabingwa hao waliopokwa na Manchester City msimu huu kumaliza ndani ya nne bora.

Ni Robert Firmino dakika ya 43, Nathaniel Phillips dakika ya 52 na Alex Oxlade Chamberlain dakika ya 88 walipachika mabao kwa Liverpool. 

Ushindi huo unaifanya Liverpool kufikisha alama 66 ikiwa nafasi ya nne baada ya kucheza mechi 37 na Burnley ipo nafasi ya 17 na pointi 39.

Ina kazi ya kushinda mchezo wake mmoja wa mwisho uliobaki ili kuweza kumaliza katika nafasi hiyo ya nne kwa kuwa mshindani wake Leicester City ambaye yupo nafasi ya tano naye pia ana pointi 66 hivyo akipoteza na mpinzani wake akashinda atashushwa hapo alipo.


SOMA NA HII  HUU HAPA MPIRA RASMI WA KOMBE LA DUNIA..UNAMBWEMBWE HATARI..SHUTI KIDOGO..KASI YA KIMONDO..