Home Azam FC AZAM FC KAMILI GADO KUIVAA BIASHARA UNITED LEO

AZAM FC KAMILI GADO KUIVAA BIASHARA UNITED LEO


AZAM FC inayonolewa na Kocha Mkuu,  George Lwandamina Mei 20 ina kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Biashara United. 


Mchezo huo utachezwa Uwanja wa Azam Complex majira ya saa 1:00 usiku unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili.


Vivier Bahati,  Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo ili kupata pointi tatu.


“Tunajua kwamba mchezo utakuwa na ushindani mkubwa na kila timu inahitaji pointi tatu hivyo tupo tayari kwa ajili ya mchezo huo. 


“Mashabiki wajitokeze kwa wingi ili kutupa sapoti na kuona namna gani tutapata matokeo ndani ya uwanja,” amesema.

Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara,  Azam FC ambayo inaye kinara wa utupiaji Bongo Prince Dube mwenye mabao 13 ipo nafasi ya tatu na pointi 57.


Inakutana na Biashara United yenye mkongwe Ramadhan Chombo ikiwa nafasi ya nne na pointi 45 zote zimecheza mechi 29.

SOMA NA HII  VIJANA WA AZAM FC WAMPA MATUMAINI LWANDAMINA