Home Azam FC VIJANA WA AZAM FC WAMPA MATUMAINI LWANDAMINA

VIJANA WA AZAM FC WAMPA MATUMAINI LWANDAMINA


 KOCHA Mkuu wa Azam FC, George Lwandamina amesema kuwa anaamini wachezaji alionao watafanya kazi nzuri itakayompa nafasi ya kuleta ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara. 


Azam FC Kwenye msimamo ipo nafasi ya tatu ikiwa imekusanya pointi zake 44 baada ya kucheza jumla ya mechi 24.


Kinara ni Yanga mwenye pointi 50 akiwa amecheza jumla ya mechi 23 huku nafasi ya pili ikiwa mikononi mwa mabingwa watetezi Simba na pointi zao ni 46.


Lwandamina amesema:”Taratibu,  hatua kwa hatua vijana wanazidi kuimarika na kuleta ushindani ndani ya Ligi,”.

SOMA NA HII  KASI YA PRINCE DUBE NI NOMA, AWAKIMBIZA KAGERE NA BOCCO