Home Habari za michezo BUMBULI : SIMBA WANA ROHO MBAYA….HAWAZUNGUMZI CHOCHOTE…WANAONA TUTAPATA PESA NYINGI…

BUMBULI : SIMBA WANA ROHO MBAYA….HAWAZUNGUMZI CHOCHOTE…WANAONA TUTAPATA PESA NYINGI…


Ikiwa kesho April 30 Vigogo katika Soka la Tanzania Yanga watakutana na Simba katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Majira ya Saa 11 jioni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Wengi wameonekana kushangazwa na ukimya wa upande wa Pili yaani Simba SC ambao watakuwa wageni katika mchezo huo.

Kwa Upande wa Wenyeji, Timu ya Yanga wao kupitia kwa Mkuu wa Idara ya Habari Hassan Bumbuli na Msemaji wao Haji Manara, kwa juma zima hili wamekuwa wakizunguka katika vyombo tofauti vya Habari kuzungumzia mechi hiyo inayovuta hisia za wapenda Soka Afrika Mashariki na Kati.

Sasa leo April 29 Kupitia kituo cha tv 3, Mkuu wa Idara ya Habari ya Yanga Hassan Bumbuli amezungumzia hali hiyo baada ya kuulizwa Swali kuhusiana na hali ya kupoa kwa Dabi ikiwa imebaki siku moja kuelekea mchezo huo.

“Unajua Dabi haiwezi kupoa sema Simba wamepoa, Simba wamekuwa na kawaida ile ya roho mbaya, inapokuja Dabi ambayo wao sio wenyeji “They dont talk”(hawazungumzi) wanaona wakitangaza mechi hii sisi kama wenyeji tutafaidika na tutapata pesa jambo ambalo sio sahihi, huwasikii kuongea lolote na hata wanapoongea ni kwa kulazimishwa na Media kubwa kama Azam kwa sababu tu Azam wanaipa Simba Pesa” amesema Bumbuli

“Sisi kwenye mechi zote dhidi yao huwa tunafanya promosheni ila inapokuja kwenye mechi inayotuhusisha sisi kama wenyeji huwa wanaamua kutozungumza” amesisitiza Bumbuli

Aidha Bumbuli ameongeza kuwa Dabi zote mbili za Msimu huu (Ngao ya Jamii na Ligi Kuu) alizunguka kwenye vyombo vya habari licha ya kuwa Dabi ya Ligi iliwahusisha Simba kama wenyeji.

SOMA NA HII  KUHUSU MKATABA WA BALEKE NA SIMBA SC....JIPYA LAIBUKA....MAZEMBE WAANZA 'CHOKOCHOKO'..