Home Habari za michezo HENOCK INONGA BAKA ATAJWA BEKI BORA MSIMU HUU…AMIMINIWA MISIFA KAMA YOTE…

HENOCK INONGA BAKA ATAJWA BEKI BORA MSIMU HUU…AMIMINIWA MISIFA KAMA YOTE…


Mshambuliaji wa Polisi Tanzania, Daruweshi Saliboko amemtaja beki wa Simba, Henock Inonga Baka kuwa ndio Beki Bora msimu huu;

“Kwa mtazamo wangu ukiniambia nitaje beki bora msimu huu basi nitasema ni Inonga, kwani nimemshuhudia uwanjani tulipocheza na Simba na pia namuangalia akicheza dhidi ya timu nyingine,” amesema Saliboko na kuongeza:

“Beki anayejiamini na anaongoza wengine, tofauti na baadhi ya tabia za wachezaji ambao wanakuwa waoga kukumbushana majukumu mmoja anapojisahau.”

Inonga Baka alisajiliwa na Simba Mwanzoni mwa msimu huu akitokea Klabu ya DC Motema Pembe ya kwao nchini Congo, ambapo toka atue klabuni hapo amefaniki kupata namba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu.


SOMA NA HII  MANJI NDANI YA BONGO