Home Habari za michezo HUU HAPA MPIRA RASMI WA KOMBE LA DUNIA..UNAMBWEMBWE HATARI..SHUTI KIDOGO..KASI YA KIMONDO..

HUU HAPA MPIRA RASMI WA KOMBE LA DUNIA..UNAMBWEMBWE HATARI..SHUTI KIDOGO..KASI YA KIMONDO..


Baada ya kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo ya Adidas kuzindua mpira rasmi utakao tumika katika michuano ya kombe la Dunia la Qatar 2022 uitwao ‘Al Rihla’ shirikisho la soka duniani FIFA limeumwagia sifa mpira huo kwa jinsi ulivyoundwa.

Mkurugenzi wa Masoko wa FIFA, Jean-Francois Pathy, amesema, Huu ni mpira wa kipekee, endelevu na wa hali ya juu kutoka kwa adidas ambao utafurahiwa na nyota watakaocheza kwenye mashindano hayo makubwa zaidi ya soka duniani yatakayofanyika nchini Qatar badae mwezi november mwaka huu.

Huu ni mpira wa 14 mfululizo ambao adidas imeunda kwa ajili ya Kombe la Dunia la FIFA na umeundwa kusaidia kasi ya mchezo, kwani unasafiri kwa kasi zaidi kuliko mpira wowote uliopata kutumika katika historia ya mashindano hayo.

Jina la ‘Al Rihla’ limetokana na neno la Kiarabu lenye maana ya ‘safari’ na umeongezewa usanifu, na bendera ya taifa mwenyeji Qatar. Mpira huo umeundwa kutoka ndani kwenda nje kwa kutumia data na majaribio makubwa yamefanyika katika maabara ya adidas, kwenye vichuguu vya upepo na uwanjani na wachezaji wa soka wenyewe.

Al Rihla unatarajiwa kutoa viwango vya juu zaidi vya usahihi na kutegemewa kwenye uwanja wa mchezo, kutokana na umbo lake jipya la paneli na muundo wa uso. Na mpira huu ni mpira wa kwanza wa Kombe la Dunia la FIFA kutengenezwa kwa wino na gundi za maji pekee.

Mkurugenzi wa Usanifu, Kandanda Graphics & Hardwear katika kampuni ya adidas Franziska Loffelmann aliongeza kusema, ‘Mchezo utakua na kasi, na kadri jinsi unavyo ongezeka kasi, usahihi na uthabiti wa mpira ndio vitu muhimu sana, hivyo muundo huu mpya unaruhusu mpira kudumisha kasi ya juu zaidi unaposafiri angani, na unatazamiwa kuleta magoli mengi zaidi.

SOMA NA HII  ISHU YA MANULA KURUDI CHAMAZI..JEMEDARI AWAIBIA SIRI MABOSI AZAM..."THAMANI YAKE NI BIL 2.3"..